Deuteronomy 33:1-6
Musa Anayabariki Makabila
1 aHii ndiyo baraka Musa mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake. 2 bAlisema: “Bwana alikuja kutoka Mlima Sinai,akachomoza kama jua juu yao
kutoka Mlima Seiri,
akaangaza kutoka Mlima Parani.
Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu
kutoka kusini,
kutoka materemko ya mlima wake.
3 cHakika ni wewe ambaye huwapenda watu,
watakatifu wako wote wamo mkononi mwako.
Miguuni pako wote wanasujudu
na kutoka kwako wanapokea mafundisho,
4 dsheria ile Musa aliyotupa sisi,
tulio milki ya kusanyiko la Yakobo.
5 eAlikuwa mfalme juu ya Yeshuruni ▼
▼ Yeshuruni maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli.
wakati viongozi wa watu walipokusanyika,
pamoja na makabila ya Israeli.
6 g“Reubeni na aishi, asife,
wala watu wake wasiwe wachache.”
Copyright information for
SwhKC