Genesis 1:1-6

Siku Sita Za Uumbaji Na Sabato

1 aHapo mwanzo Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na dunia.
2 bWakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mwenyezi Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

3 cMwenyezi Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. 4 dMwenyezi Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mwenyezi Mungu akatenganisha nuru na giza. 5 eMwenyezi Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6 fMwenyezi Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.”
Copyright information for SwhKC