Isaiah 63:11-14


11 aNdipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita,
siku za Musa na watu wake:
yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari,
pamoja na wachungaji wa kundi lake?
Yuko wapi yule aliyeweka
Roho wake Mtakatifu katikati yao,

12 baliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu
kuwa katika mkono wa kuume wa Musa,
aliyegawa maji ya bahari mbele yao,
ili kujipatia jina milele,

13 caliyewaongoza kupitia kwenye vilindi?
Kama farasi katika nchi iliyo wazi,
wao hawakujikwaa,

14 dkama ng’ombe washukao bondeni kwenye malisho,
walipewa pumziko na Roho wa Bwana.
Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako
ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.

Copyright information for SwhKC