Job 21:1-6
Ayubu Anajibu: Waovu Mara Nyingi Huenda Bila Kuadhibiwa
1Ndipo Ayubu akajibu:2 a“Yasikilizeni maneno yangu kwa makini;
hii na iwe faraja mnayonipa mimi.
3 bNivumilieni ninapozungumza,
nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki.
4 c“Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu?
Kwa nini nisikose subira?
5 dNiangalieni mkastaajabu;
mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu.
6 eNinapowaza juu ya hili, ninaogopa,
nao mwili wangu unatetemeka.
Copyright information for
SwhKC