Joshua 1:1-6
Bwana Anamwagiza Yoshua
1 aBaada ya kifo cha Musa mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Musa: 2 b“Mtumishi wangu Musa amekufa. Sasa basi, wewe pamoja na watu wote hawa, jiandaeni kuvuka huu Mto Yordani kuingia nchi ambayo karibu nitawapa wana wa Israeli. 3 cKila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Musa. 4 dNchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa ▼▼ Yaani Bahari ya Mediterania.
iliyoko upande wa magharibi. 5 fHakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia. 6 g“Uwe hodari na shujaa, kwa sababu wewe ndiwe utakayewaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa.
Copyright information for
SwhKC