Joshua 19:32-37

32Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo: 33 aMpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mti mkubwa ulio katika Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani. 34 bMpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki. 35 cMiji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, 36 dAdama, Rama, Hazori, 37 eKedeshi, Edrei, na En-Hasori,
Copyright information for SwhKC