Joshua 22:1-6

Makabila Ya Mashariki Yarudi Nyumbani

1 aNdipo Yoshua akawaita Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, 2 bnaye akawaambia, “Mmeshafanya yale yote Musa mtumishi wa Bwana aliyowaamuru, nanyi mmenitii kwa kila jambo nililowaamuru. 3Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kazi Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliyowapa. 4 cSasa kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ile ambayo Musa mtumishi wa Bwana aliwapa ng’ambo ya Yordani. 5 dLakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria zile Musa mtumishi wa Bwana alizowapa: yaani kumpenda Bwana Mwenyezi Mungu wenu na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.”

6 eNdipo Yoshua akawabariki na kuwaaga waende zao, nao wakaenda nyumbani mwao.
Copyright information for SwhKC