Leviticus 3:1-6

Sadaka Ya Amani

1 a“ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ng’ombe kutoka kundi, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Bwana. 2 bAtaweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Haruni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. 3 cKutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani, 4figo zote pamoja na mafuta yote yanayozizunguka karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. 5 dKisha wana wa Haruni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

6 e“ ‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kama sadaka ya amani kwa Bwana, atamtoa dume au jike asiye na dosari.
Copyright information for SwhKC