Mark 3:20-25

20 aKisha Isa aliporudi nyumbani, umati wa watu ukakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula. 21 bNdugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”

22 cWalimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli!
Beelzebuli kwa Kiyunani ni Beelzebubu, yaani mkuu wa pepo wachafu.
Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!”

23 eBasi Isa akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani? 24Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama. 25Nayo nyumba kama ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
Copyright information for SwhKC