Romans 6:1-6

Kufa Na Kufufuka Pamoja Na Al-Masihi

1 aTuseme nini basi? Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka? 2 bLa hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutawezaje kuendelea kuishi tena katika dhambi? 3 cAu hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Al-Masihi Isa tulibatizwa katika mauti yake? 4 dKwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Al-Masihi alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima.

5 eKwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo wake. 6 fKwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi.
Copyright information for SwhKC