1 Chronicles 12:23-28

23 aHawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kama Bwana alivyokuwa amesema: 24watu wa Yuda, wanaochukua ngao na mikuki walikuwa 6,800 wote wakiwa tayari kwa vita.
25Watu wa Simeoni, mashujaa waliokuwa tayari kwa vita walikuwa 7,100.
26Watu wa Lawi walikuwa 4,600, 27pamoja na Yehoyada, kiongozi wa jamaa ya Haruni, aliyekuwa pamoja na watu 3,700, 28 bna Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake.
Copyright information for SwhKC