1 Kings 8:9-14

9Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili za mawe ambazo Musa alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo Bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.

10Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la Bwana. 11Nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu lake.

12Ndipo Sulemani akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene; 13 anaam, hakika nimekujengea Hekalu zuri sana, mahali pako pa kuishi milele.”

Hotuba Ya Sulemani

(2 Nyakati 6:3-11)

14Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki.
Copyright information for SwhKC