2 Kings 4:8-13

8 aSiku moja Al-Yasa akaenda Shunemu. Huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo, ambaye alimsisitiza Al-Yasa aje kula chakula. Kwa hiyo kila mara alipitia pale, akaingia humo ili ale. 9Akamwambia mumewe, “Ninajua kwamba huyu mtu ambaye anakuja kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu. 10 bTutengeneze chumba kidogo juu darini na tuweke ndani yake kitanda na meza, kiti na taa kwa ajili yake. Kisha anaweza kukaa humo kila mara akija kwetu.”

11Siku moja Al-Yasa alipofika, akapanda chumbani kwake na kulala humo. 12 cAkamwambia mtumishi wake Gehazi, “Mwite huyo Mshunami.” Hivyo akamwita, naye akaja akasimama mbele yake. 13Al-Yasa akamwambia mtumishi wake, “Mwambie huyu mwanamke, ‘Umetaabika sana kwa ajili yetu. Sasa utendewe nini? Je, tunaweza kuzungumza na mfalme au jemadari wa jeshi kwa niaba yako?’ ”

Akajibu, “Mimi ninaishi kwangu miongoni mwa watu wangu.”

Copyright information for SwhKC