2 Kings 5:1-6

Naamani Aponywa Ukoma

1 aWakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, Bwana alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari shujaa, lakini alikuwa na ukoma.
Ukoma ni neno lililotumika kwa Kiebrania kueleza magonjwa mbalimbali ya ngozi ambayo si lazima yawe ni ukoma halisi.

2 cSiku hizo vikosi kutoka Aramu vilikuwa vimekwenda na vikawa vimemteka msichana kutoka Israeli, naye akamtumikia mkewe Naamani. 3Akamwambia bibi yake, “Kama bwana wangu angelimwona nabii aliyeko Samaria! Angemponya ukoma wake.”

4Naamani akaenda kwa bwana wake na kumwambia alichosema yule msichana kutoka Israeli. 5 dMfalme wa Aramu
Yaani mfalme wa Shamu.
akamjibu, “Hakika, nenda. Nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo Naamani akaondoka, akiwa amechukua talanta kumi
Talanta 10 za fedha ni sawa na kilo 340.
za fedha, shekeli 6,000 za dhahabu,
Shekeli 6,000 za dhahabu ni sawa na kilo 70.
na mivao kumi ya mavazi.
6Barua aliyopelekea mfalme wa Israeli iliandikwa hivi: “Pamoja na barua hii ninamtuma mtumishi wangu, Naamani, kwako ili uweze kumponya ukoma wake.”

Copyright information for SwhKC