Ezekiel 31:1-6

Mwerezi Katika Lebanoni

1 aKatika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema: 2 b“Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake ya wajeuri: “ ‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa
na wewe katika fahari.

3 cAngalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni,
ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli;
ulikuwa mrefu sana,
kilele chake kilipita majani ya miti yote.

4 dMaji mengi yaliustawisha,
chemchemi zenye maji mengi ziliufanya urefuke;
vijito vyake vilitiririka pale
ulipoota pande zote
na kupeleka mifereji yake
kwenye miti yote ya shambani.

5 eHivyo ukarefuka
kupita miti yote ya shambani;
vitawi vyake viliongezeka
na matawi yake yakawa marefu,
yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji.

6 fNdege wote wa angani
wakaweka viota kwenye vitawi vyake,
wanyama wote wa shambani
wakazaana chini ya matawi yake,
mataifa makubwa yote
yaliishi chini ya kivuli chake.
Copyright information for SwhKC