Ezekiel 43:1-6

Utukufu Warudi Hekaluni

1 aKisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki, 2 bnami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikang’aa kwa utukufu wake. 3 cMaono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. 4 dUtukufu wa Bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki. 5 eKisha Roho akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa Bwana ulilijaza Hekalu.

6 fWakati yule mtu akiwa amesimama kando yangu, nilisikia mtu mmoja akisema nami kutoka ndani ya Hekalu.
Copyright information for SwhKC