Genesis 29:31-35

31Bwana alipoona kwamba Lea hapendwi, akampa watoto, lakini Raheli alikuwa tasa. 32Lea akapata mimba akazaa mwana. Akamwita Reubeni,
Reubeni maana yake Ona mwana, yaani Yehova ameangalia taabu yangu.
kwa maana alisema, “Ni kwa sababu Bwana ameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.”

33Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Kwa sababu Bwana alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita Simeoni.
Simeoni maana yake Anasikia, yaani sasa ataungana nami kama Raheli.

34Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Sasa afadhali mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita Lawi.
Lawi maana yake Nimeunganishwa, yaani na mume wangu.

35Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifu Bwana.” Kwa hiyo akamwita Yuda.
Yuda maana yake Sifa, yaani Nitamsifu Yehova.
Kisha akaacha kuzaa watoto.
Copyright information for SwhKC