Genesis 38:1-6

Yuda Na Tamari

1Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake akaenda kuishi na Hira Mwadulami. 2Huko Yuda akakutana na binti wa Kikanaani aitwaye Shua akamwoa na akakutana naye kimwili, 3akapata mimba akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri. 4Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita Onani. 5Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita Shela. Huyu alimzalia mahali paitwapo Kezibu.

6Yuda akampatia Eri, mzaliwa wake wa kwanza mke, aitwaye Tamari.
Copyright information for SwhKC