Isaiah 60:3-8
3 aMataifa watakuja kwenye nuru yako
na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.
4 b“Inua macho yako na utazame pande zote:
Wote wanakusanyika na kukujia,
wana wako wanakuja toka mbali,
nao binti zako wanabebwa mikononi.
5 cNdipo utatazama na kutiwa nuru,
moyo wako utasisimka na kujaa furaha,
mali zilizo baharini zitaletwa kwako,
utajiri wa mataifa utakujilia.
6 dMakundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako,
ngamia vijana wa Midiani na Efa.
Nao wote watokao Sheba watakuja,
wakichukua dhahabu na uvumba
na kutangaza sifa za Bwana.
7 eMakundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,
kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia,
watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu,
nami nitalipamba Hekalu langu tukufu.
8 f“Ni nani hawa warukao kama mawingu,
kama hua kuelekea kwenye viota vyao?
Copyright information for
SwhKC