Jeremiah 48:1-6
Ujumbe Kuhusu Moabu
1 aKuhusu Moabu: Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa.Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa;
Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa.
2 bMoabu haitasifiwa tena;
huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake:
‘Njooni na tuangamize taifa lile.’
Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa;
upanga utakufuatia.
3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu,
kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.
4 Moabu utavunjwa,
wadogo wake watapiga kelele.
5 cWanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi,
wakilia kwa uchungu wanapotembea,
kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu,
kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.
6 dKimbieni! Okoeni maisha yenu,
kuweni kama kichaka jangwani.
Copyright information for
SwhKC