John 17:1-6

Isa Ajiombea Mwenyewe

1 aBaada ya Isa kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema:

“Baba, saa imewadia. Umtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe.

2

bKwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa.

3

cNao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Isa Al-Masihi uliyemtuma.

4

dNimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye.

5

eHivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwepo.

Isa Awaombea Wanafunzi Wake

6 f“Nimelidhihirisha jina lako kwa wale ulionipa kutoka ulimwengu. Walikuwa wako, nawe ukanipa mimi, nao wamelitii neno lako.
Copyright information for SwhKC