John 18:1-6

Isa Akamatwa

(Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Luka 22:47-53)

1 aIsa alipomaliza kuomba, akaondoka na wanafunzi wake wakavuka Bonde la Kidroni. Upande wa pili palikuwa na bustani, yeye na wanafunzi wake wakaingia humo.

2 bBasi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Isa alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara. 3 cHivyo Yuda akaja bustanini. Aliongoza kikosi cha askari wa Kirumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha.

4 dIsa akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?”

5 eWao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.”

Isa akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
6Isa alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini!

Copyright information for SwhKC