Luke 1:60-63

60 aLakini mama yake akakataa na kusema, “Hapana! Jina lake ataitwa Yahya.”

61Wakamwambia, “Hakuna mtu yeyote katika jamaa yako mwenye jina kama hilo.”

62 bBasi wakamfanyia Zekaria baba yake ishara ili kujua kwamba yeye angependa kumpa mtoto jina gani. 63 cAkaomba wampe kibao cha kuandikia na kwa mshangao wa kila mtu akaandika: “Jina lake ni Yahya.”
Copyright information for SwhKC