Luke 3:2-7
2 anao Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, neno la Mungu likamjia Yahya, mwana wa Zekaria huko jangwani. 3 bAkaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 4 cKama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aliaye nyikani,‘Itengenezeni njia ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.
5 Kila bonde litajazwa,
kila mlima na kilima vitashushwa.
Njia zilizopinda zitanyooshwa,
na zilizoparuza zitasawazishwa.
6 dNao watu wote watauona
wokovu wa Mungu.’ ”
7 eYahya akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?
Copyright information for
SwhKC