Matthew 27:45-50

45 aTangu saa sita hadi saa tisa giza liliifunika nchi yote. 46 bIlipofika saa tisa, Isa akapaza sauti akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

47Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama pale waliposikia hayo, wakasema, “Anamwita Ilya.”

48 cGhafula mmoja wao akaenda mbio na kuleta sifongo, akaichovya kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Isa ili anywe. 49Wengine wakasema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Ilya atakuja kumwokoa.”

50 dIsa alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake.

Copyright information for SwhKC