Matthew 5:38-43

38 a“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 bLakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia. 40 cKama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia. 41 dKama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili. 42 eMpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.

Upendo Kwa Adui

(Luka 6:27-28, 32-36)

43 f“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’
Copyright information for SwhKC