Psalms 59:1-6
Kuomba Ulinzi Wa Mungu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Usiharibu. Utenzi Wa Daudi. Wakati Sauli Alipotuma Wapelelezi Nyumbani Mwa Daudi Ili Wamuue)
1 a bEe Mungu, uniokoe na adui zangu,
unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu.
2 cUniponye na watu watendao mabaya,
uniokoe kutokana na wamwagao damu.
3 dTazama wanavyonivizia!
Watu wakali wananifanyia hila,
ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea
wala kutenda dhambi.
4 eSijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia.
Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya!
5 fEe Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli!
Zinduka uyaadhibu mataifa yote,
usionyeshe huruma kwa wasaliti.
6 gHurudi wakati wa jioni,
wakibweka kama mbwa,
wakiuzurura mji.
Copyright information for
SwhKC