1 Chronicles 20

Kutekwa Kwa Raba

1Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme hutoka kwenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni akaenda Raba na kuuzunguka huo mji kwa Jeshi, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akaushambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu. 2Daudi akachukua taji kutoka kwenye kichwa cha mfalme wao, uzito wake ulikuwa talanta moja
20.2 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34
ya dhahabu na ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua kiasi kikubwa cha nyara kutoka katika mji huo
3na akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.

Vita Na Wafilisti

4Baada ya muda, kulitokea vita dhidi ya Wafilisti, huko Gezeri. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamwua Sipai, aliyekuwa mmoja wa wazao wa Warefai
20.4 Yaani majitu
, nao Wafilisti wakashindwa.

5Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.

6Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuweko na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu, jumla ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai. 7Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamwua.

8Hawa walikuwa ndio wazao wa Mrefai huko Gathi, nao walianguka kwa mkono wa Daudi na watu wake.

Copyright information for Neno