1 Chronicles 23

Jamaa Za Walawi Na Utendaji Wao

Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Solomoni mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.

Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000. Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la BWANA na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi, na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu BWANA kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”

Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

Wagerishoni

Wana wa Wagerishoni walikuwa wawili:
  • Ladani na Shimei.
Wana wa Ladani walikuwa watatu: Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli. Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomothi 23.9 Yaani Shelomithi; maana yake ni Mpenda amani , Hazieli na Harani. Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani. 10 Nao wana wa Shimei walikuwa wanne: Yahathi, Ziza 23.10 Tafsiri zingine zinamwita Zina , Yeushi na Beria. 11 Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja. Wakohathi 12 Wana wa Kohathi walikuwa wanne:
  • Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
13 Wana wa Amramu walikuwa: Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vile vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za BWANA, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la BWANA milele. 14 Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi. 15 Wana wa Mose walikuwa: Gershomu na Eliezeri. 16 Wazao wa Gershomu: Shubaeli alikuwa wa kwanza. 17 Wazao wa Eliezeri: Rehabia alikuwa wa kwanza. Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana. 18 Wana wa Ishari: Shelomithi alikuwa wa kwanza. 19 Wana wa Hebroni walikuwa: Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu. 20 Wana wa Uzieli walikuwa: Mika wa kwanza na Ishia wa pili. Wamerari 21 Wana wa Merari walikuwa:
  • Mahli na Mushi.
  • Wana wa Mahli walikuwa:
  • Eliyazari na Kishi.
22 Eliyazari akafa bila kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa. 23 Wana wa Mushi: Mahli, Ederi na Yerimothi; wote walikuwa watatu. 24 Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la BWANA. 25 Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile BWANA, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele, 26 Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo cho chote cha utumishi wake.” 27 Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri miaka ishirini au zaidi.

28 Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la BWANA: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wo wote katika nyumba ya Mungu. 29 Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa. 30 Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu BWANA. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni 31 na wakati wo wote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa BWANA siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamuriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za BWANA mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.

32 Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la BWANA.

Copyright information for Neno