1 Chronicles 25

Waimbaji

Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:

Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa:

Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme.

Wana wa Yeduthuni walikuwa sita:

Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza BWANA.

Wana wa Hemani walikuwa:

Bukia, Matania, Uzieli, Shubaeli na Yerimothi, Hanania, Hanani, Eliyatha, Gidalti na Romanti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi.
Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la BWANA wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme. Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa BWANA. Idadi yao walikuwa 288.
Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, wanawe na jamaa zake, 12 Ya pili ikamwangukia Gedalia, yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12 10 Ya tatu ikamwangukia Zakuri, wanawe na jamaa zake, 12 11 ya nne ikamwangukia Isri 25.11 Isri jina lingine ni Seri , wanawe na jamaa zake, 12 12 ya tano ikamwangukia Nethania, wanawe na jamaa zake, 12 13 ya sita ikamwangukia Bukia, wanawe na jamaa zake, 12 14 ya saba ikamwangukia Yesarela 25.14 Yesarela jina lingine ni Asarela , wanawe na jamaa zake, 12 15 ya nane ikamwangukia Yeshaya, wanawe na jamaa zake, 12 16 ya tisa ikamwangukia Matania, wanawe na jamaa zake, 12 17 ya kumi ikamwangukia Shimei, wanawe na jamaa zake, 12 18 ya kumi na moja ikamwangukia Azareli 25.18 Azareli jina lingine ni Uzieli , wanawe na jamaa zake, 12 19 ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia, wanawe na jamaa zake, 12 20 ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli, wanawe na jamaa zake, 12 21 ya kumi na nne ikamwangukia Matithia, wanawe na jamaa zake, 12 22 ya kumi na tano ikamwangukia Yerimothi, wanawe na jamaa zake, 12 23 Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania, wanawe na jamaa zake, 12 24 ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha, wanawe na jamaa zake, 12 25 ya kumi na nane ikamwangukia Hanani, wanawe na jamaa zake, 12 26 ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi, wanawe na jamaa zake, 12 27 ya ishirini ikamwangukia Eliyatha, waanawe na jamaa zake, 12 28 ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri, wanawe na jamaa zake, 12 29 ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti, wanawe na jamaa zake, 12 30 ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi, wanawe na jamaa zake, 12 31 ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri, wanawe na jamaa zake, 12.
Copyright information for Neno