1 Chronicles 6

Wana Wa Lawi

1Wana wa Lawi walikuwa:
  • Gershoni, Kohathi na Merari.
2Wana wa Kohathi walikuwa: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. 3Amramu alikuwa na wana: Aroni, Mose, na Miriamu. Aroni alikuwa na wana: Nadabu, Abihu, Eliyazari na Ithamari. 4Eliyazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua, 5Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, 6Uzi akamzaa Zerahia, Zerahia akamzaa Merayothi, 7Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, 8Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi, 9Ahimaasi akamzaa Azaria, Azaria akamzaa Yohanani, 10Yohanani akamzaa Azaria (ndiye aliyefanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu), 11Azaria akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, 12Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Shalumu, 13Shalumu akamzaa Hilkia, Hilkia akamzaa Azaria, 14Azaria akamzaa Seraya, Seraya akamzaa Yehosadaki. 15Yehosadaki alihamishwa wakati BWANA alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza. 16Wana wa Lawi walikuwa: Gershoni, Kohathi na Merari. 17Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni: Libni na Shimei. 18Wana wa Kohathi walikuwa: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. 19Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao: 20Wazao wa Gershoni: Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, Yahathi akamzaa Zima, 21Zima akamzaa Yoa, Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera, Zera akamzaa Yeatherai. 22Wazao wa Kohathi: Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora, Kora akamzaa Asiri, 23Asiri akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri, 24Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli, Urieli akamzaa Usia, Usia akamzaa Shauli. 25Wazao wa Elikana walikuwa: Amasia na Ahimothi, 26Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai, Sofai akamzaa Nahathi, 27Nahathi akamzaa Eliyabu, Eliyabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Samweli. 28Wana wa Samweli walikuwa: Yoeli mzaliwa wake wa kwanza na Abiya mwanawe wa pili. 29Wafuatao ndio wazao wa Merari: Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza, 30Uza akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaia. Waimbaji Wa Hekalu 31Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya BWANA baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la BWANA huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

33Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:
  • Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:
  • Hemani, mpiga kinanda,
  • alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
34mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa, 35mwana wa Zufu, mwana wa Elikana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai, 36mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania, 37mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, 38mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli; 39na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume: Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea, 40mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya, 41mwana wa Ethni, mwana wa Zera, mwana wa Adaia, 42mwana wa Ethani, mwana wa Zima, mwana wa Shimei, 43mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi. 44Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto ni: Elthani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki, 45mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia, 46mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri, 47mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi. 48Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu. 49Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu. 50

  • Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni:
  • Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,
  • Finehasi akamzaa Abishua,
51Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Serahia, 52Serahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, 53Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi. 54Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao. (Walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

55Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka. 56Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.

57Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, 58Hileni, Debiri, 59Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. 60Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.

Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.

61Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.

62Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

63Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

64Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho. 65Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.

66Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.

67Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, 68Yokmeamu, Beth-Horoni 69Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.

70Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki wa miji ya Eneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.71Wagerishoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho:
  • Katika nusu ya kabila la Manase:
  • walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.
72Kutoka kabila la Isakari walipokea Kedeshi, Daberathi, 73Ramoth na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho. 74Kutoka kabila la Asheri walipokea Mashali, Abdoni, 75Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho. 76Kutoka kabila la Naftali walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho. 77Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo: kutoka kabila la Zabuloni walipokea Yokneamu, Karta, Rimono na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho. 78Kutoka kabila la Reubeni, ng'ambo ya Yordani mashariki ya Yeriko walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahsa, 79Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho. 80Na kutoka kabila la Gadi walipokea Ramoth huko Gileadi, Mahanaimu, 81Heshboni na Yezeri pamoja na maeneo yake ya malisho.
Copyright information for Neno