Acts 8
1Naye Sauli alikuwepo pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano.Kanisa Lateswa Na Kutawanyika
Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya kanisa huko Yerusalemu, waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria. 2Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana. 3Lakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatia gerezani.Filipo Ahubiri Injili Samaria
4Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda. 5Filipo akatelemkia mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Kristo ▼▼8:5 Yaani Masiya
. 6Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza aliyofanya, wakasikiliza kwa bidii yale aliyosema. 7Pepo wachafu wakawa wakiwatoka watu wengi huku wakipiga kelele na wengi waliopooza na viwete wakaponywa. 8Hivyo pakawa na furaha kuu katika mji huo.Simoni, Mchawi
9Basi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kwamba yeye ni mtu mkuu, 10watu wote wakubwa kwa wadogo wakamsikiliza na kumaka wakisema “Mtu huyu ndiye uweza wa Mungu ujulikanao kama ‘Uweza Mkuu.’ ” 11Wakamfuata kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake. 12Lakini watu walipomwamini Filipo akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, wakabatizwa wanaume na wanawake. 13Simoni naye akaamini na akabatizwa. Akamfuata Filipo kila mahali, akistaajabishwa na ishara kuu na miujiza aliyoiona.14Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria wamelipokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana waende huko. 15Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho Mtakatifu, 16kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa bado hajawashukia hata mmoja ila wamebatizwa tu katika jina la Bwana Yesu. 17Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea Roho Mtakatifu.
18Simoni alipoona kuwa watu wanapokea Roho Mtakatifu mitume walipoweka mikono juu yao, akawapa fedha 19akisema, “Nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayeweka mikono yangu juu yake apate kupokea Roho Mtakatifu.”
20Petro akamjibu, “Fedha yako na iangamie pamoja nawe, kwa sababu ulidhani unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha! 21Wewe huna sehemu wala fungu katika huduma hii kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. 22Kwa hiyo tubia huu uovu wako na umwombe Mungu, ili yamkini, aweze kusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako. 23Kwa maana ninaona kwamba wewe umejawa na uchungu na ni mfungwa wa dhambi.”
24Ndipo Simoni akajibu, “Niombeeni kwa Bwana, ili hayo mliyosema lo lote lisinitukie.”
25Nao walipokwisha kutoa ushuhuda na kuhubiri neno la Bwana, wakarudi Yerusalemu wakihubiri injili katika vijiji vingi vya Samaria.
Filipo Na Towashi Wa Kushi
26Basi Malaika wa Bwana akamwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza ambayo ni jangwa.” 27Hivyo akaondoka na kwenda. Akiwa njiani akakutana na towashi wa Kushi, aliyekuwa afisa mkuu, mwenye mamlaka juu ya hazina zote za Kandake, Malkia wa Kushi. Huyu towashi alikuwa amekwenda Yerusalemu ili kuabudu, 28naye akiwa njiani kurudi nyumbani alikuwa ameketi garini mwake akisoma kitabu cha nabii Isaya. 29Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye lile gari ukae karibu nalo.”30Ndipo Filipo akakimbilia lile gari na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamwuliza, “Je, unaelewa hayo usomayo?”
31Yule towashi akasema, “Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?” Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye.
32Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la maandiko: “Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni,
kama mwana-kondoo anyamazavyo
mbele yake yeye amkataye manyoya,
hivyo hakukifungua kinywa chake.
33Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake.
Nani awezaye kueleza juu ya kizazi chake?
Kwa maana maisha yake yameondolewa
kutoka duniani.”
34Yule towashi akamwuliza Filipo, “Tafadhali niambie, nabii huyu anena kwa habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?” 35Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la maandiko akamweleza habari njema za Yesu.
36Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, yule towashi akamwambia Filipo, “Tazama, hapa kuna maji. Kitu gani kitanizuia nisibatizwe?” ( 37Filipo akamwambia, “Kama ukiamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu).” 38Naye akaamuru lile gari lisimamishwe. Wakatelemka kwenye maji wote wawili, yule towashi na Filipo, naye Filipo akambatiza. 39Nao walipopanda kutoka kwenye maji, ghafula Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, naye towashi hakumwona tena, lakini akaenda zake akifurahi. 40Filipo akajikuta yuko Azoto, akasafiri akihubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.
Copyright information for
Neno