Deuteronomy 5
Amri Kumi
1Mose akawaita Israeli wote, akawaambia:Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata. 2BWANA Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu. 3Si kwamba BWANA alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo. 4BWANA alisema nanyi uso kwa uso kutoka katika moto juu ya mlima. 5(Wakati huo nilisimama kati ya BWANA na ninyi kuwatangazia neno la BWANA, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:
6“Mimi ndimi BWANA Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka katika nchi ya utumwa. 7
- Usiwe na miungu mingine ila mimi.
23Mliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi. 24Nanyi mkasema, “BWANA Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. 25Lakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya BWANA Mungu wetu zaidi. 26Ni mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi? 27Sogea karibu usikie yale yote asemayo BWANA Mungu wetu. Kisha utuambie cho chote kile ambacho BWANA Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”
28BWANA aliwasikia wakati mlipozungumza nami, na BWANA akaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri. 29Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!
30“Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao. 31Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.”
32Hivyo iweni waangalifu kuyafanya yale BWANA Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto. 33Fuateni yale yote ambayo BWANA Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.
Copyright information for
Neno