Ecclesiastes 5

Simama Katika Kicho Cha Mungu

Linda hatua zako uendapo katika nyumba ya Mungu. Karibia usikilize kuliko kutoa dhabihu ya wapumbavu, ambao hawajui kuwa wanafanya kosa. Usiwe mwepesi kuzungumza,
usiwe na haraka katika moyo wako
kuzungumza lo lote mbele za Mungu.
Mungu yuko mbinguni
nawe uko duniani,
kwa hiyo maneno yako
na yawe machache.
Kama vile ndoto huja
wakati kuna shughuli nyingi,
ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu
wakati kuna maneno mengi.Wakati unapomwekea Mungu nadhiri, usikawie kuitimiza. Yeye hafurahii wapumbavu; timiza nadhiri yako. Ni afadhali usiweke nadhiri kuliko kuiweka na usiitimize. Usiruhusu kinywa chako kukuingiza dhambini. Tena usijitetee mbele ya huyo mjumbe wa hekaluni, ukisema, “Niliweka nadhiri kwa makosa.” Kwa nini Mungu akasirike kwa ajili ya yale unayosema na kuiharibu kazi ya mikono yako? Kuota ndoto kwingi na maneno mengi ni ubatili. Kwa hiyo simama katika kicho cha Mungu.

Utajiri Ni Ubatili

Kama ukiona maskini wanaonewa katika nchi, hukumu na haki vikipotoshwa, usishangazwe na mambo hayo, kwa maana afisa mmoja anaangaliwa na aliye juu yake zaidi na juu ya hao wawili kuna wengine walio juu zaidi yao. Mafanikio ya nchi ni kwa ajili ya wote, hata mfalme mwenyewe hufaidi kutoka mashambani. 10 Ye yote apendaye fedha kamwe
hatosheki na fedha;
ye yote apendaye utajiri kamwe
hatosheki na kipato chake.
Hili nalo pia ni ubatili.
11 Mali ikiongezeka, ndivyo walaji
wanavyoongezeka.
Hii nayo inamfaidia nini mwenye mali
isipokuwa ni kushibisha macho yake?
12 Usingizi wa kibarua ni mtamu,
awe amekula kidogo au kingi,
lakini wingi wa mali
humnyima tajiri usingizi.13 Nimeshaona uovu mzito chini ya jua: Utajiri uliolimbikizwa kwa kujinyima
na kuleta madhara kwa mwenye mali,
14 au utajiri uliopotea kwa bahati mbaya,
hivyo kwamba wakati akiwa na mwana
hakuna cho chote kilichobaki kwa ajili yake.
15 Mtu hutoka tumboni mwa mama yake uchi,
naye jinsi alivyokuja vivyo hivyo huondoka.
Hachukui cho chote kutokana na kazi yake
ambacho anaweza kukibeba mkononi mwake.16 Hili nalo ni baya la kusikitisha: Kama vile mtu ajavyo, vivyo hivyo huondoka,
naye anapata faida gani,
maadamu hutaabika kwa ajili ya upepo?
17 Siku zake zote hula gizani,
pamoja na fadhaa kubwa,
mateso na hasira.18 Ndipo nikatambua kwamba ni vyema na sahihi kwa mtu kula na kunywa na kutosheka katika kazi yake ngumu chini ya jua katika siku chache za maisha yake Mungu alizompa, kwa maana hili ndilo fungu lake. 19 Zaidi ya yote, Mungu anapompa mtu ye yote utajiri na milki, humwezesha kuvifurahia, kukubali fungu lake na kuwa na furaha katika kazi yake, hii ni karama ya Mungu. 20 Mara chache mtu huzifikiri siku za maisha yake, kwa sababu Mungu humfanya ashikwe na furaha ya moyoni.

Copyright information for Neno