Esther 10

Ukuu Wa Mordekai

1Mfalme Ahusuero alitoza ushuru katika ufalme wake wote hadi kwenye miambao yake ya mbali. 2Matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amemkuza, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Umedi na Uajemi? 3Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo kutoka Mfalme Ahusuero, naye alikuwa bora kabisa miongoni mwa Wayahudi, alipandishwa katika heshima ya juu na ndugu zake Wayahudi kwa sababu aliwatendea mema watu wake na alizungumza kwa ajili ya ustawi wa Wayahudi wote.

Copyright information for Neno