Exodus 36

Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtu BWANA aliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vile BWANA alivyoagiza.”

Ndipo Mose akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye BWANA alikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi. Wakapokea kutoka kwa Mose sadaka zote ambazo Waisraeli walikuwa wameleta ili kuifanya kazi ya ujenzi wa Mahali Patakatifu. Nao watu wakaendelea kuleta sadaka za hiari kila asubuhi. Ikafika wakati mafundi wote wenye ujuzi waliokuwa wakiifanya kazi yote ya mahali patakatifu wakasimamisha kazi zao ili kuja kumwambia Mose, “Watu wanaleta zaidi kuliko mahitaji kwa ajili ya kazi hii ambayo BWANA ameagiza ifanyike.”

Ndipo Mose akatoa agizo, nao wakapeleka neno hili katika kambi yote: “Mtu ye yote mwanaume au mwanamke asilete tena kitu cho chote kwa ajili ya sadaka ya mahali patakatifu.” Hivyo watu wakazuiliwa kuleta zaidi, kwa sababu walivyokuwa navyo tayari vilitosha na kuzidi kuifanya kazi yote.

Maskani Ya Mungu

Watu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, pamoja na makerubi yaliyotariziwa juu yake na fundi stadi. Mapazia yote yalikuwa yamelingana: kila moja lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane
36.9 Dhiraa 28 ni sawa na mita 12.6
na upana wa dhiraa nne
36.9 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8
.
10 Wakayaunganisha mapazia matano pamoja, pia wakafanya hivyo hivyo kwa yale mengine matano. 11 Kisha wakatengeneza vitanzi vya buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, na vitanzi vingine katika pazia la mwisho la kipande cha pili. 12 Wakatengeneza pia vitanzi hamsini katika pazia la kipande cha kwanza, na vitanzi vingine hamsini mwishoni mwa pazia la pili na vitanzi vyote vikaelekeana. 13 Kisha wakatengeneza vibanio hamsini vya dhahabu, na wakavitumia kufunga na kuunganisha vile vipande viwili vya pazia pamoja ili maskani ipate kuwa kitu kimoja.

14 Wakatengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya hema juu ya maskani. 15 Mapazia yote kumi na moja yalikuwa yamelingana, urefu wa dhiraa thelathini
36.15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5
na upana wa dhiraa nne.
16 Wakaunganisha mapazia matano pamoja na yale mengine sita pamoja. 17 Kisha wakatengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwishoni la kipande cha kwanza, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwishoni la kipande cha pili. 18 Wakatengeneza vibanio hamsini vya shaba ili kulikaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. 19 Kisha wakatengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi laini za wanyama.

20 Wakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 21 Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi
36.21 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5
na upana wa dhiraa moja na nusu
36.21 Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5
,
22 zikiwa na ndimi mbili kila mmoja sambamba na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani kwa njia hii. 23 Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, 24 na wakatengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuwekwa chini yake, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. 25 Kwa upande wa kaskazini wa maskani wakatengeneza mihimili ishirini 26 na vitako arobaini vya shaba, viwili chini ya kila mhimili. 27 Wakatengeneza mihimili sita kwa ajili ya upande wa mwisho, yaani upande wa magharibi wa maskani, 28 na mihimili miwili ikatengenezwa kwa ajili ya pembe za maskani za upande wa mwisho. 29 Katika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa jozi moja kuanzia chini mpaka juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; jozi zote mbili zilikuwa za kufanana. 30 Kwa hiyo kulikuwa na mihimili minane na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila kizingiti.

31 Wakatengeneza pia mataruma kwa mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, 32 matano kwa ajili ya yale yaliyo upande mwingine, na matano kwa ajili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa wa maskani. 33 Wakatengeneza taruma la katikati, likapenya katikati ya mihimili kutoka upande mmoja hadi mwingine. 34 Wakaifunika hiyo mihimili kwa dhahabu, na wakatengeneza pete za dhahabu za kushikilia hayo mataruma. Pia wakayafunika yale mataruma kwa dhahabu.

35 Wakatengeneza mapazia kwa nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu kwa kitani iliyosokotwa vizuri, yakiwa yametariziwa makerubi na fundi stadi. 36 Wakatengeneza nguzo nne za mti wa mshita kwa ajili yake na kuzifunika kwa dhahabu. Wakatengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili yake na kusubu vitako vinne vya fedha. 37 Kwa ajili ya ingilio la hema wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi; 38 pia wakatengeneza nguzo tano zenye kulabu. Wakafunika ncha za juu za hizo nguzo kwa dhahabu pamoja na tepe zake, pia wakatengeneza vitako vyake vitano vya shaba.

Copyright information for Neno