Exodus 37

Sanduku La Agano

1Bezaleli akatengeneza Sanduku kwa mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu
37.1 Dhiraa moja na nusu ni sawa na mita 1.13
, upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu.
2Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu. 3Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na nyingine mbili upande mwingine. 4Kisha akatengeneza mipiko kwa mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 5Akaiingiza ile mipiko ndani ya zile pete kwenye pande za Sanduku ili kulibeba.

6Akatengeneza kifuniko cha upatanisho kwa dhahabu safi: urefu wake dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. 7Kisha akatengeneza makerubi mawili kwenye miisho ya kile kifuniko kutokana na dhahabu iliyofuliwa. 8Akaweka kerubi moja mwisho huu na kerubi la pili mwisho mwingine; akayafanya kuwa kitu kimoja na hicho kifuniko. 9Mabawa ya makerubi yalikuwa yaliyokunjuliwa kuelekea juu, yakitilia kifuniko uvuli. Makerubi yalielekeana, yakitazama kuelekea kifuniko.

Meza

10Akatengeneza meza ya mbao za mshita urefu wake dhiraa mbili
37.10 Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90
, upana wake dhiraa moja
37.10 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45
na kimo chake dhiraa moja na nusu.
11Kisha akaifunika kwa dhahabu safi na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka. 12Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne
37.12 Nyanda nne ni sawa na sentimita 8
kuizunguka ile meza na kuuweka ukingo wa dhahabu juu yake.
13Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya ile meza na kuzifungia kwenye pembe zake nne, pale penye miguu minne ya meza. 14Pete hizo ziliwekwa karibu na ile duara ya upapi ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. 15Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu. 16Vyombo vyote vya mezani vilitengenezwa kwa dhahabu safi; yaani, sahani zake, masinia, mabakuli na magudulia kwa ajili ya kumiminia sadaka za kinywaji.

Kinara Cha Taa

17Akatengeneza kinara cha taa kwa dhahabu safi iliyofuliwa vizuri, kitako chake na ufito, vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa vya kitu kimoja. 18Matawi sita yalijitokeza kwenye pande za kile kinara cha taa, matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. 19Vikombe vyenye muundo wa maua ya mlozi vikiwa na matovu na maua kwenye tawi moja, vitatu vilikuwa kwenye tawi lililofuata na yanayofanana na matawi yote sita yalitokeza kwenye kile kinara cha taa. 20Juu ya kinara kulikuwepo na vikombe vinne vyenye muundo kama maua ya mlozi, vikiwa na matovu yake na maua yake. 21Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyojitokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani, jumla matawi sita. 22Matovu na matawi vyote vilikuwa kitu kimoja na kinara cha taa, kikiwa kimefuliwa kwa dhahabu safi.

23Akatengeneza taa zake saba, mikasi ya kusawazishia tambi pamoja na masinia ya dhahabu safi. 24Akatengeneza kinara hicho cha taa pamoja na vifaa vyake vyote kutoka kwenye talanta
37.24 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34
moja ya dhahabu safi.

Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba

25Akatengeneza madhabahu ya kufukiza uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu wake dhiraa moja, upana wake dhiraa moja, na kimo chake dhiraa mbili: pembe zake zilikuwa za kitu kimoja nayo. 26Sehemu ya juu ya meza pande zake zote pamoja na zile pembe zilifunikwa kwa dhahabu safi, pia akazitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka. 27Akatengeneza pete mbili za dhahabu chini ya huo ukingo, mbili kila upande, ili zishikilie ile mipiko iliyobebea hiyo madhabahu. 28Akatengeneza mipiko kwa miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu.

29Pia akatengeneza mafuta matakatifu ya upako na uvumba safi, wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato.

Copyright information for Neno