Exodus 38

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa

Akatengeneza madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa mbao za mti wa mshita, kimo chake dhiraa tatu;
38.1 Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35
nayo ilikuwa mraba, urefu wake dhiraa tano na upana wa dhiraa tano
38.1 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25
.
Akatengeneza upembe kwenye kila pembe katika hizo pembe nne, ili kwamba zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, akafunika madhabahu kwa shaba. Akatengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, nyuma za nyama na sufuria za kuchukulia moto. Akatengeneza wavu wa shaba, uwe chini ya ukingo wa madhabahu ili kwamba ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. Akasubu pete za shaba za kushikilia ile mipiko kwa ajili ya pembe nne za huo wavu wa shaba. Akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuifunika kwa shaba. Akaingiza ile mipiko kwenye zile pete, ili hiyo mipiko iwe upande huu na upande huu wa madhabahu kwa ajili ya kuibeba. Akaitengeneza madhabahu yenye uvungu ndani yake akitumia mbao.

Sinia La Kunawia

Akatengeneza sinia la shaba na kitako chake cha shaba kutokana na vioo vya shaba vilivyotolewa na wanawake waliohudumu penye ingilio la Hema la Kukutania.

Ua Wa Kukutania

Kisha akatengeneza ua ambao upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa 100
38.9 Dhiraa 100 ni sawa na mita 45
na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
10 wenye nguzo ishirini na vitako ishirini vya shaba, pia zilikuwa na kulabu za fedha na tepe za fedha juu yake. 11 Upande wa kaskazini ulikuwa pia na urefu wa dhiraa mia moja, na ulikuwa na wenye nguzo ishirini na vitako ishirini vya shaba, pamoja na kulabu za fedha na tepe za fedha juu yake.

12 Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini
38.12 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5
na ulikuwa na mapazia, pamoja na nguzo kumi na vitako kumi, pamoja na kulabu za fedha na tepe za fedha juu yake.
13 Upande wa mwisho wa mashariki linakotokea jua, pia kulikuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano
38.14 Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75
yalikuwa upande mmoja wa ingilio pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu,
15 mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yalikuwa upande mwingine wa ingilio kuelekea kwenye ua, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16 Mapazia yote yaliyozunguka ua yalikuwa ya kitani iliyosokotwa vizuri. 17 Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, ncha zake zilifunikwa kwa fedha, kwa hiyo nguzo yote ya ua ilikuwa na tepe za fedha.

18 Pazia la kwenye ingilio la ua lilikuwa la kitani lililosokotwa vizuri la rangi ya buluu, ya zambarau, na nyekundu, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama yale ya kwenye ua, kwenda juu kwake lilikuwa dhiraa tano, 19 pakiwa na nguzo nne na vitako vinne vya shaba. Kulabu zake na tepe zake zilikuwa za fedha, ncha zake zilikuwa zimefunikwa kwa fedha. 20 Vigingi vyote vya maskani vilivyozunguka ua vilikuwa vya shaba.

Vifaa Vilivyotumika

21 Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani, maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Mose, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Aroni. 22 (Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, alifanya kila kitu BWANA alichomwamuru Mose, 23 akiwa pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, fundi stadi wa kutia nakshi, kubuni michoro, mtarizi kwa rangi ya buluu, ya zambarau, nyekundu na kitani safi.) 24 Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta 29 na shekeli 730
38.24 Talanta 29 na shekeli 730 ni sawa na tani moja
, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.

25 Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli 1,775
38.25 Talanta 100 na shekeli 1,775 za fedha ni sawa na tani 3.4
, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
26 Kila mtu alitoa beka moja, ambayo ni sawa na nusu shekeli ya fedha, kwa kazi ya mahali patakatifu, kutoka kwa kila mtu aliyekuwa amehesabiwa mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi, ambao jumla yao walikuwa wanaume 603,550. 27 Talanta hizo 100 za fedha zilitumika kusubu vile vitako mia moja kwa ajili ya mahali patakatifu na mapazia, vitako mia moja kwa talanta mia, yaani, talanta moja kwa kila kitako. 28 Akatumia zile shekeli hizo 1,775 kutengeneza kulabu za nguzo, kufunika ncha za nguzo na kutengeneza vitanzi vyake.

29 Shaba iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa ilikuwa na uzito wa talanta 70 na shekeli 2,400
38.29 Talanta 70 na shekeli 2,400 ni sawa na tani 2.4
30 Akaitumia hiyo shaba kutengeneza vitako vya ingilio la Hema la Kukutania, madhabahu ya shaba pamoja na ule wavu wake na vyombo vyake vyote, 31 vile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya Maskani pamoja na ule ua uliozunguka.

Copyright information for Neno