Ezra 2

Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni

Basi hawa ndio watu wa jimbo, waliotoka uhamishoni ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirejea Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):

Orodha ya watu wa Israeli ilikuwa:wazao wa Paroshi 2,172 wa Shefatia 372 wa Ara 775 wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812 wa Elamu 1,254 wa Zatu 945 wa Zaka 760 10 wa Bani 642 11 wa Bebai 623 12 wa Azgadi 1,222 13 wa Adonikamu 666 14 wa Bigwai 2,056 15 wa Adini 454 16 wa Ateri (kwa Hezekia) 98 17 wa Besai 323 18 wa Yora 112 19 wa Hashumu 223 20 wa Gibari 95 22 wa Netofa 56 23 wa Anathothi 128 24 wa Azmawethi 42 25 wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743 26 wa Rama na Geba 621 27 wa Mikmashi 122 28 wa Betheli na Ai 223 29 wa Nebo 52 30 wa Magbishi 156 31 wa Elamu ile ingine 1,254 32 wa Harimu 320 33 wa Lodi, Hadidi na Ono 725 34 wa Yeriko 345 35 wa Senaa 3,630
36 

Makuhani:

37 wa Imeri 1,052 38 wa Pashuri 1,247 39 wa Harimu 1,017
40 

Walawi:

41 

Waimbaji:

42 

Mabawabu wa lango la Hekalu:

43 

Wanethini
2.43 Yaani watumishi wa Hekalu (pia 2:58, 70)
:
  • wazao wa
  • Siha, Hasufa, tabaothi,
44 Kerosi, Siaha, Padoni, 45 Lebana, Hagaba, Akubu, 46 Hagabu, Shalmai, Hanani, 47 Gideli, Gahari, Reaya, 48 Resini, Nekoda, Gazamu, 49 Uza, Pasea, Besai, 50 Asna, Meunimu, Nefusimu, 51 Bakbuki, Hakufa, Harhuri, 52 Basluthi, Mehida, Harsha, 53 Barkosi, Sisera, Tema, 54 Nesia na Hatifa. 55 Wazao wa watumishi wa Solomoni:
  • wazao wa
  • Sotai, Hasaferethi, Peruda,
56 Yaala, Darkoni, Gideli, 57 Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami. 58 Wanethini na wazao wa watumishi wa Solomoni 392
59 

Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuonyesha ya kuwa jamaa zao zilitokana na uzao wa Israeli:

60 Wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 652 61 

Kutoka miongoni mwa makuhani:
  • Wazao wa
  • Hobaya, Hakosi, Barzilai (ambaye alikuwa ameoa binti wa Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo.)


62 Hawa walitafuta orodha ya jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kwenye kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63 Mtawala aliwaagiza wasile chakula cho chote kitakatifu mpaka awepo kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu
2.63 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha
.64 Kundi lote lilikuwa na watu 42,360; 65 pamoja na hao kulikuwapo na watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwapo waimbaji wanaume na wanawake 200. 66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, 67 ngamia 435 na punda 6,720.68 Walipofika kwenye nyumba ya BWANA huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika lile eneo lake. 69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000
2.69 Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500
za dhahabu, mane 5,000
2.69 Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900
za fedha na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hii.

70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na Wanethini waliishi mijini mwao, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi kwenye miji yao.

Copyright information for Neno