Ezra 1

Koreshi Asaidia Watu Kurudi Kutoka Uhamishoni

1Katika mwaka wa kwanza wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kutimiza neno la BWANA lililosemwa na Yeremia, BWANA aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote na kuliweka katika maandishi:

2“Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:

“ ‘BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za duniani na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda.
3Ye yote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la BWANA, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko huko Yerusalemu. 4Nao watu wa mahali po pote wale walionusurika wanapoishi sasa, watu hao wampe fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, mbali na sadaka za hiari kwa ajili ya Hekalu la Mungu huko Yerusalemu.’ ”5Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya BWANA huko Yerusalemu. 6Majirani zao wote wakawasaidia vyombo vya fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, pia na zawadi za thamani, pamoja na sadaka zote za hiari. 7Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu la BWANA, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalua la mungu wake. 8Koreshi mfalme wa Uajemi akavitoa kwa mkono wa Mithredathi mtunza hazina, aliyevihesabu mbele ya Sheshbaza mkuu wa Yuda.

9Hii ilikuwa ndio orodha ya vifaa:

10mabakuli ya dhahabu yalikuwa 30 mabakuli ya fedha yanayofanana yalikuwa 410 vifaa vingine vilikuwa 1,000. 11

Kwa ujumla, kulikuweko na vyombo 5,400 vya dhahabu na vya fedha. Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.

Copyright information for Neno