Genesis 2

1Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo. 2
  • Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote.
3Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya. Adamu Na Eva 4Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.

BWANA Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
5hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa BWANA Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, 6lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: 7BWANA Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi
2:7 Neno la Kiebrania la mavumbi ya ardhi ndilo kiini cha jina la mwanadamu wa kwanza, Adamu
ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, mtu akawa kiumbe hai.

8Basi BWANA Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. 9BWANA Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne. 11Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. 12(Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, lulu na vito shohamu pia hupatikana huko.) 13Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. 14Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Eufrati.

15BWANA Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. 16BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wo wote katika bustani, 17lakini kamwe usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”

18BWANA Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

19Basi BWANA Mungu alikuwa amefanyiza kutoka katika ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lo lote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. 20Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini.

Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa.
21Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. 22Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

23Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu
na nyama ya nyama yangu,
ataitwa ‘mwanamke
2:23 Jina la Kiebrania la mwanamke linafanana na lile la mwanaume
,’
kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”24Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

25Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.

Copyright information for Neno