Isaiah 13

Unabii Dhidi Ya Babeli

Neno kuhusu Babeli ambalo Isaya mwana wa Amozi aliliona: Twekeni bendera juu ya mlima usio na kitu,
wapazieni sauti,
wapungieni mkono waingie
katika malango ya wenye heshima.
Nimewaamuru watakatifu wangu;
nimewaita mashujaa wangu
waitimize hasira yangu:
wale wanaoshangilia ushindi wangu.
Sikilizeni kelele juu ya milima,
kama ile ya umati mkubwa wa watu!
Sikilizeni, makelele katikati ya falme,
kama mataifa yanayokusanyika pamoja!
BWANA Mwenye Nguvu Zote anakusanya
jeshi kwa ajili ya vita.
Wanakuja kutoka nchi za mbali sana,
kutoka miisho ya mbingu,
BWANA na silaha za ghadhabu yake,
kuangamiza nchi yote.
Ombolezeni, kwa maana siku ya BWANA i karibu,
itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi
13:6 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania
.
Kwa sababu ya hili, mikono yote italegea,
moyo wa kila mtu utayeyuka.
Hofu itawakamata,
uchungu na maumivu makali yatawashika,
watajinyonganyonga kama mwanamke
aliye na utungu wa kuzaa.
Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake,
nyuso zao zikiwa katika hali
ya kuwaka kama moto.
Tazameni, siku ya BWANA inakuja,
siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali,
kuifanya nchi kuwa ukiwa
na kuwaangamiza wenye dhambi
waliomo ndani yake.
10 Nyota za mbinguni na makundi ya nyota
havitatoa mwanga wake.
Jua linalochomoza litatiwa giza
na mwezi hautatoa nuru yake.
11 Nitauadhibu ulimwengu kwa ajili ya uovu wake,
waovu kwa ajili ya dhambi zao.
Nitakomesha majivuno ya wenye kiburi
Na nitakishusha kiburi cha watu wakatili.
12 Nitawafanya wanadamu kuwa adimu
kuliko dhahabu safi,
watakuwa wachache sana
kuliko dhahabu ya Ofiri.
13 Kwa hiyo nitazifanya mbingu zitetemeke,
nayo dunia itatikisika kutoka mahali pake
katika ghadhabu ya BWANA Mwenye Nguvu Zote,
katika siku ya hasira yake iwakayo.
14 Kama swala awindwaye,
kama kondoo wasio na mchungaji,
kila mmoja atarudi kwa watu wake mwenyewe,
kila mmoja atakimbilia nchi yake ya kuzaliwa.
15 Ye yote atakayetekwa atapasuliwa tumbo,
wote watakaokamatwa watauawa kwa upanga.
16 Watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande
mbele ya macho yao;
nyumba zao zitatekwa
na wake zao watatendwa jeuri.
17 Tazama, nitawachochea Wamedi dhidi yao,
ambao hawajali fedha
wala hawafurahii dhahabu.
18 Mishale yao itawaangusha vijana,
hawatakuwa na huruma kwa watoto wachanga
wala hawataangalia watoto kwa huruma.
19 Babeli, johari ya falme,
utukufu wa kiburi cha Wababeli
13.19 Wababeli hapa maana yake ni Wakaldayo
,
itaangushwa na Mungu
kama Sodoma na Gomora.
20 Hautakaliwa na watu kamwe
wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote,
hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko,
hakuna mchungaji atakayepumzisha
makundi yake ya kondoo
na mbuzi huko.
21 Lakini viumbe wa jangwani watalala huko,
mbweha watajaza nyumba zake,
bundi wataishi humo
nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo.
22 Fisi watalia ndani ya ngome zake,
mbweha ndani ya majumba yake
ya kifalme ya fahari.
Wakati wake umewadia,
na siku zake hazitaongezwa.


Copyright information for Neno