Isaiah 27

Wokovu Kwa Ajili Ya Israeli

1Katika siku ile, BWANA ataadhibu kwa upanga wake,
upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu,
ataadhibu Lewiathani
27.1 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa
yule nyoka apitaye mbio kwa mwendo laini,
Lewiathani yule nyoka mwenye kupindapinda;
atamwua joka huyo mkubwa sana wa baharini.2Katika siku ile: “Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:
3Mimi, BWANA, ninalitunza,
nitalinyweshea maji mfululizo.
Ninalichunga mchana na usiku ili mtu ye yote asije akalidhuru.
4Mimi sijakasirika.
Hata kama pangekuwepo michongoma
na miiba inayonikabili!
Ningepambana dhidi yake katika vita,
ningeliichoma moto yote.
5Au niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,
wao na wafanye amani nami,
naam, wafanye amani nami.”
6Katika siku zijazo Yakobo atatia mizizi,
Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,
naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.
7Je, BWANA amempiga kama alivyowapiga wale waliompiga?
Je, yeye ameuawa
kama wale waliouawa
ambao walimwua yeye?
8Kwa vita na kwa kumfukuza unapingana naye,
kwa mshindo wake mkali anamfukuza,
kama siku uvumapo upepo wa mashariki.
9Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho,
hili litakuwa ndiyo matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake:
Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu
kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande,
hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia
uvumba zitakazobaki zimesimama.
10Mji ulio na boma umebaki ukiwa,
makao yaliyotelekezwa yameachwa kama jangwa,
huko ndama hulisha,
huko hujilaza,
wanakwanyua matawi yake.
11Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa
nao wanawake huja na kuwasha navyo moto.
Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu,
kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao,
Muumba wao hawaonyeshi fadhili.12Katika siku ile BWANA atapura kutoka matiririko ya mto wa Eufrati hadi Kijito cha Misri, nanyi, Ee Waisraeli mtakusanywa pamoja mmoja mmoja. 13Katika siku ile tarumbeta kubwa italia. Wale waliokuwa wakiangamia katika nchi ya Ashuru, nao wale waliokuwa uhamishoni katika nchi ya Misri watakuja na kumwabudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

Copyright information for Neno