Isaiah 8

Ashuru, Chombo Cha BWANA

BWANA akaniambia, “Chukua gombo kubwa uandike juu yake kwa kalamu ya kawaida. Maher-Shalal-Hash-Bazi
8.1 Maher-Shalal-Hash-Bazi maana yake ni Haraka kuteka nyara, Upesi kwenye hizo nyara
.
Nami nitawaita kuhani Uria na Zekaria mwana wa Yeberekia kama mashahidi wangu waaminifu.”

Kisha nikaenda kwa nabii mke, naye akapata mimba akazaa mwana. Kisha BWANA akaniambia, “Mwite huyo mtoto Maher-Shalal-Hash-Bazi. Kabla mtoto hajaweza kusema, ‘Baba yangu’ au ‘Mama yangu,’ utajiri wa Dameski na nyara za Samaria zitachukuliwa na mfalme wa Ashuru.”

BWANA akasema nami tena: “Kwa sababu watu hawa wamekataa maji ya Shilo yatiririkayo taratibu
wakamfurahia Resini na mwana wa Remalia,
kwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao
mafuriko makubwa ya Mto
8.7 Yaani Eufrati
,
mfalme wa Ashuru na fahari yake yote.
Yatafurika juu ya mifereji yake yote,
yatamwagikia juu ya kingo zake zote
na kufika hadi Yuda, ukizunguka kwa kasi juu yake,
yakipita kutoka upande huu
mpaka upande mwingine yakifika hadi shingoni.
Mabawa yake yaliyokunjuliwa
yatafunika upana wa nchi yako,
Ee Imanueli
8:8 Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi
!”
Inueni kilio cha vita, enyi mataifa
na mkavunjwevunjwe!
Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali.
Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
10 Wekeni mikakati yenu, lakini itashindwa;
fanyeni mipango yenu, lakini haitafanikiwa,
kwa maana Mungu yu pamoja nasi
8:10 Kiebrania ni Imanueli
.


Mwogope Mungu

11 BWANA alisema nami mkono wake wenye nguvu ukiwa juu yangu, akinionya nisifuate njia za taifa hili. Akasema: 12 “Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina,
usiogope kile wanachokiogopa,
wala usikihofu.
13 BWANA Mwenye Nguvu Zote ndiye peke yake
ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu,
ndiye peke yake utakayemwogopa,
ndiye peke yake utakayemhofu,
14 naye atakuwa mahali patakatifu;
lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa
jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa
na mwamba wa kuwaangusha.
Kwa watu wa Yerusalemu atakuwa
mtego na tanzi.
15 Wengi wao watajikwaa;
wataanguka na kuvunjika,
watategwa na kunaswa.”
16 Funga ushuhuda na
kutia muhuri sheria
miongoni mwa wanafunzi wangu.
17 Nitamngojea BWANA,
ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake.
Nitaliweka tumaini langu kwake.18 Nipo hapa pamoja na watoto ambao BWANA amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa BWANA Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.

19 Wakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunong'ona na kunung'unika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai? 20 Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko. 21 Wakiwa na dhiki na njaa, watazunguka katika nchi yote, watakapotaabika kwa njaa, watapatwa na hasira kali, wakiwa wanatazama juu, watamlaani mfalme wao na Mungu wao. 22 Kisha wataangalia duniani na kuona dhiki na giza, hofu na huzuni tupu, nao watasukumiwa kwenye giza nene kabisa.

Copyright information for Neno