Jeremiah 22

Hukumu Dhidi Ya Wafalme Waovu

Hili ndilo asemalo BWANA: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na utangaze ujumbe huu huko: ‘Sikia neno la BWANA, Ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi, wewe, maafisa wako na watu wako mnaokuja kwa kupitia malango haya. Hili ndilo BWANA asemalo: Tenda kwa haki na kwa adili. Mwokoe kutoka mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane wal a usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa. Kwa kuwa kama ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao. Lakini kama hukuyatii maagizo haya, asema BWANA, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ”

Kwa kuwa hili ndilo BWANA asemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda: “Ingawa uko kama Gileadi kwangu,
kama kilele cha Lebanoni,
hakika nitakufanya uwe kama jangwa,
kama miji ambayo haijakaliwa na watu.
Nitawatuma waharabu dhidi yako,
kila mtu akiwa na silaha zake,
nao watazikata boriti zako nzuri za mierezi
na kuzitupa motoni.“Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini BWANA amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’ Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha Agano la BWANA, Mungu wao na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ” 10 

Usimlilie yeye aliyekufa wala usimwombolezee;
badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu
yule aliyepelekwa uhamishoni,
kwa sababu kamwe hatairudia
wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.11 Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Shalumu
22.11 Shalumu ndiye pia anaitwa Yehoahazi
mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “yeye kamwe hatarudi tena.
12 Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka, hataiona tena nchi hii.” 13 

“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme
kwa njia ya dhuluma,
vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,
akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,
bila kuwalipa kwa utumushi wao.
14 Asemaye, ‘Nitajijengea jumba kubwa la kifalme
na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’
Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,
huweka mbao za mierezi
na kuipamba kwa rangi nyekundu.
15 “Je, inakufanya kuwa mfalme
kwa kuongeza idadi ya mierezi?
Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?
Alifanya yaliyo sawa na haki,
hivyo yeye akafanikiwa katika yote.
16 Aliwatetea maskini na wahitaji,
hivyo yeye akafanikiwa katika yote,
Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”
asema BWANA.
17 “Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu
katika mapato ya udhalimu,
kwa kumwaga damu isiyo na hatia,
kwa uonevu na ukatili.”18 Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: “Hawatamwombolezea wakisema:
‘Ole, ndugu yangu! Ole umbu langu!’
Hawatamwombolezea wakisema:
‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’
19 Atazikwa maziko ya punda:
ataburutwa na kutupwa
nje ya malango ya Yerusalemu.”
20 “Panda Lebanoni ukapige kelele,
sauti yako na isikike huko Bashani,
piga kelele toka Abarimu, kwa kuwa
wale wote waliojiunga nawe
wameangamizwa.
21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,
lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’
Hii imekuwa ndiyo kawaida yako tangu ujana wako;
hujanitii mimi.
22 Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,
wale ulioungana nao
watakwenda uhamishoni.
Kisha utaaibika na kufedheheka kwa sababu
ya uovu wako wote.
23 Wewe uishiye Lebanoni,
wewe uliyetulia
kwenye majengo ya mierezi,
tazama jinsi utakavyoomboleza
maumivu makali yatakapokupata,
maumivu kama yale ya mwanamke
mwenye utungu wa kuzaa!24 “Hakika kama niishivyo,” asema BWANA, “hata kama wewe, Yekonia
22.24 Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini
mwana wa Yehoyakimu
22.24 Yehoyakimu ni jina jingine la Yehoyakini
mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekung'oa utoke hapo.
25 Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. 26 Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. 27 Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.” 28 

Je, huyu Yekonia ni mtu aliyedharauliwa,
chungu kilichovunjika,
tena chombo kisichotakiwa na mtu ye yote?
Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,
na kutupwa kwenye nchi wasioijua?
29 Ee nchi, nchi, nchi,
sikia neno la BWANA!
30 Hili ndilo BWANA asemalo:
“Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto,
mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote,
kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa,
kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi
wala kuendelea kutawala katika Yuda.”


Copyright information for Neno