Jeremiah 43

Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote ya BWANA Mungu wao, kila kitu BWANA alichokuwa amemtuma kuwaambia, Azaria mwana wa Hoshaya na Yohanani mwana wa Karea na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo! BWANA Mungu wetu hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’ Lakini Baruki mwana wa Neria anakuchochea wewe dhidi yetu ili ututie mikononi mwa Wakaldayo, ili watuue au watuchukue uhamishoni Babeli.”

Basi Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi na watu wote wakakataa kutii amri ya BWANA ya kukaa katika nchi ya Yuda. Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka katika mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa. Pia wakawaongoza wanaume wote, wanawake na watoto na binti za mfalme ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa kifalme alikuwa amewaacha pamoja na Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani na nabii Yeremia na Baruki mwana wa Neria. Kwa hiyo wakaingia Misri kwa kutokumtii BWANA na wakaenda mpaka Tahpanhesi
43.7 Tahpanhesi ni mji katika nchi ya Misri
.

Huko Tahpanhesi neno la BWANA likamjia Yeremia kusema: “Wakati Wayahudi wakiwa wanaona, chukua baadhi ya mawe makubwa na kuyazika katika udongo wa mfinyanzi katika njia iliyojengwa kwa matofali katika ingilio la jumba la kifalme la Farao huko Tahpanhesi. 10 Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha enzi juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza chandarua yake ya kifalme juu yake. 11 Atakuja na kuishambulia Misri, akiwaua wale waliokusudiwa kuuawa, aweteke mateka wale waliokusudiwa kutekwa na upanga kwa wale waliokusudiwa upanga. 12 Atachoma moto mahekalu yao ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama vile mchungaji ajizungushiavyo vazi lake ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo bila kudhurika. 13 Humo ndani ya hekalu la jua
43:13 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua)
katika Misri atabomoa nguzo za ibada na kuteketeza kwa moto mahekalu ya miungu wa Misri.’ ”

Copyright information for Neno