Jeremiah 45

Ujumbe Kwa Baruki

Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruki mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruki kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule: “Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruki: Ulisema, ‘Ole wangu! BWANA ameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ”

BWANA akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Nitakibomoa kile nilichokijenga na kung'oa kile nilichokipanda, katika nchi yote. Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo. Kwa kuwa nitaleta maangamizi juu ya watu wote, asema BWANA, lakini po pote utakapokwenda nitayaokoa maisha yako.’ ”

Copyright information for Neno