Job 26

Hotuba Ya Tisa Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Utukufu Wa Mungu Hauchunguziki

Kisha Ayubu akajibu: “Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!
Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!
Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?
Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha!
Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?
Nayo ni roho ya nani iliyosema
kutoka kinywani mwako?
“Wafu wako katika maumivu makuu,
wale walio chini ya maji
na wale waishio ndani yake.
Mauti
26.6 Yaani Kuzimu; kwa Kiebrania ni Abadon ambayo maana yake ni sawa na Sheol
iko wazi mbele za Mungu;
uharibifu haukufunikwa.
Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu,
naye huining'iniza dunia mahali pasipo na kitu.
Huyafungia maji kwenye mawingu yake,
hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
Huufunika uso wa mwezi mpevu,
akitandaza mawingu juu yake.
10 Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji,
ameweka mpaka wa nuru na giza.
11 Nguzo za mbingu nazo zatetemeka,
zinatishika anapozikemea.
12 Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari,
kwa hekima yake
alimkata Rahabu
26.12 Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa
vipande vipande.
13 Aliisafisha anga kwa pumzi yake,
kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.
14 Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake,
tazama jinsi ulivyo mdogo mnong'ono tunaousikia kumhusu!
Ni nani basi awezaye kuelewa
ngurumo za nguvu zake?”


Copyright information for Neno