Jonah 2

Maombi ya Yona Katika Tumbo la Nyangumi

1Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba BWANA Mungu wake. 2Akasema: “Katika shida yangu nalimwita BWANA,
naye akanijibu.
Kutoka kina cha kaburi
2.2 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol
niliomba msaada,
nawe ukasikiliza kilio changu.
3Ulinitupa kwenye kilindi,
ndani kabisa ya moyo wa bahari,
mikondo ya maji ilinizunguka,
mawimbi yako yote na viwimbi
vilipita juu yangu.
4Nikasema, ‘Nimefukuziwa
mbali na uso wako,
hata hivyo nitatazama tena
kuelekea Hekalu lako takatifu.’
5Maji yaliyonimeza yalinitisha,
kilindi kilinizunguka;
mwani
2.5 Mwani hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu ya kilindi cha bahari
ulijisokota kichwani pangu.
6Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,
makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.
Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,
Ee BWANA Mungu wangu.
7“Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka,
nilikukumbuka wewe, BWANA,
nayo maombi yangu yalikufikia wewe,
katika Hekalu lako takatifu.
8“Wale watu wanaong'ang'ana na sanamu zisizofaa
hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.
9Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,
nitakutolea dhabihu.
Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.
Wokovu watoka kwa BWANA.”10Basi BWANA akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

Copyright information for Neno