Joshua 12

Orodha Ya Wafalme Walioshindwa

Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli walikuwa wamewashinda na kutawala nchi yao upande wa mashariki ya Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:Sihoni mfalme wa Waamori,

ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ni pamoja na nusu ya Gileadi.
Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi
12.3 Yaani Bahari ya Galilaya
hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi
12:3 Yaani Bahari Mfu
), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya matelemko ya Pisga.

Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani,

aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa Wageshuri, Wamaaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.Mose mtumishi wa BWANA na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi wa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ulioelekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:
nchi ya vilima, nchi chini ya vilima, upande wa magharibi, Araba, matelemko ya mlima, jangwa, na Negebu; watu waliokuwa wanaishi katika maeneo haya walikuwa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):mfalme wa Yeriko mmoja mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja 10 mfalme wa Yerusalemu mmoja mfalme wa Hebroni mmoja 11 mfalme wa Yarmuthi mmoja mfalme wa Lakishi mmoja 12 mfalme wa Egloni mmoja mfalme wa Gezeri mmoja 13 mfalme wa Debiri mmoja mfalme wa Gederi mmoja 14 mfalme wa Horma mmoja mfalme wa Aradi mmoja 15 mfalme wa Libna mmoja mfalme wa Adulamu mmoja 16 mfalme wa Makeda mmoja mfalme wa Betheli mmoja 17 mfalme wa Tapua mmoja mfalme wa Heferi mmoja 18 mfalme wa Afeki mmoja mfalme wa Lasharoni mmoja 19 mfalme wa Madoni mmoja mfalme wa Hazori mmoja 20 mfalme wa Shimron-Meroni mmoja mfalme wa Akshafu mmoja 21 mfalme wa Taanaki mmoja mfalme wa Megido mmoja 22 mfalme wa Kedeshi mmoja mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja 23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) 12:23 Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori mmoja mfalme wa Goyimu katika Gilgali mmoja 24 mfalme wa Tirsa mmoja wafalme jumla yao walikuwa thelathini na mmoja.
Copyright information for Neno